Evelyn Acham anataka shule za Uganda kuongeza somo la mabadiliko ya hali ya hewa kwa mtaala wao

Marielle Issa  | 

(Courtesy of Evelyn Acham)

(Courtesy of Evelyn Acham)

Mwanaharakati wa Uganda anajadili hitaji la elimu ya hali ya hewa na kuangazia sauti za Kiafrika katika vita vya kupigania mazingira.

Mwulize mwanaharakati wa mabadiliko ya hali ya hewa wa Uganda Evelyn Acham alikojifunza kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Ilikuwa ni wakati rafiki yake Vanessa Nakate alipoingia kwenye taarifa za kimataifa mwaka jana kwa kauli ya maandamano ya mwanamke mmoja jijini Kampala, mji mkuu wa Uganda. “Alienda mbele ya Bunge jambo lililokuwa la kijasiri na lenye kutia moyo,” Evelyn anasema. Niliendelea kumwambia nitajiunga nawe, ninataka kujua kile unachofanya, nalo lilinitia moyo kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.” 

Akiwa na hamu ya kujiunga na rafiki yake katika vita vya kupigania mazingira na kamwe hajawahi kujifunza kuhusu somo hili shuleni, Evelyn alijisajili kwa kozi za mtandaoni zinazohusu upunguzaji wa gesi chafu na maendeleo endelevu. “Kwa kuona shauku na nguvu alizokuwanazo [Vanessa] kuhusu sayari hii, lilinisukuma sana kurudi nyuma na kusoma,” Evelyn anasema. Kidogo, alianza kuona madhara ya ongezeko la joto ulimwenguni kila mahali karibu naye. Hewa ya Kampala ilikuwa imechafuka. Jiji liling’oa miti. Mimea ya kijani kibichi iliyoifunika Uganda hapo awali sasa inapatikana tu katika maeneo ya mashambani.

Ikiwa kwenye ikweta, Uganda inayo moja ya hali za hewa zinazobadilika kwa haraka sana. Joto linapoongezeka, Mafuriko na kiangazi vinatishia mimea inayotegemea mvua ambayo familia za mashambani kama ya Evelyn zinategemea. Matatizo yamezidi, na Evelyn anahofia kuwa shule za Uganda hazijafanya juhudi za kutosha kwa kuwatayarisha vijana kwa siku za usoni. “Mfumo wa elimu haukunitendea haki,” aliiambia Agenda ya Wanawake mnamo Mei kwamba, “Uganda haishughulikii haki za hali ya hewa na uwajibikaji.” 

Mfumo wa elimu haukunitendea haki. Uganda haishughulikii haki za hali ya hewa na uwajibikaji.
— Evelyn Acham

Kwa Evelyn, kujumuisha elimu ya hali ya hewa katika mtaala ni muhimu ili kuhakikisha vijana wa Uganda wanakua na ufahamu muhimu wa kuhifadhi mazingira. “Mawazo yao yangali kwenye mchakato wa kujifunza, kupokea na kukubali kile wanasikia,” anasema. “Mtu hawezi kufanya jambo lolote ikiwa hana maarifa kulihusu.” Evelyn anajua ya kwamba kuleta madiliko darasani kunaanza na hatua za kiserikali kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na elimu juu ya hali ya hewa. “Watu wanaendelea kupanda miti sasa, lakini sheria na kanuni hazibadiliki. Bado hatujaliona hilo,” anaeleza. “Shule zinaweza tu kufuata yale viongozi wameandaa.” 

Akichochewa na maarifa aliyopata kutoka kwa masomo yake, Evelyn alijiunga na vikundi vya vijana wanaotetea hali ya hewa. Yeye ni wanachama hai wa chama cha Vijana kwa Afrika Ijayo na mratibu wa kitaifa wa Vuguvugu la Amka nchini Uganda, Evelyn hupanga maandamano ya hali ya hewa, kampeni za kidijitali, Uzoaji wa takataka na ziara za shuleni, yote hayo kwa lengo la kuleta hamasisho la hali ya hewa nchini Uganda. “Nina imani kuwa watu wengi zaidi hawajafahamishwa,” anasema. “Watu hawawezi kutenda jambo kwa kile hawajui.”

Hivi majuzi, Evelyn ameangaziwa kimataifa kutokana na kazi yake. Msimu huu alizungumza kama mmoja wa Webina ya Wanawake Wachanga Wanaoongoza Shughuli za Kutetea Hali ya Hewa naye aliwasili kama mgeni rasmi kwenye kikao cha Watu wa Sayari hii pamoja na Vanessa. Mnamo Julai, alizungumza katika Kongamano la Mabadiliko la Ulimwengu (Impact Global Summit) la MUN, hafla ya siku tatu iliyopangwa na Umoja wa Mataifa. Mapema mwaka huu, Evelyn alifanyika kuwa mwanachama wa mtandao wa wanaharakati wa Arctic Angels, tukio ambalo anasema limemsukuma kufikiria kuhusu hali ya hewa ulimwenguni kote na kupanua mipaka yake kama wakili. “Kinachoathiri Afrika kinaathiri maaeneo mengine ya Ulimwengu,” anaeleza. “Kinachofanyika Aktiki hakisalii tu huko.” 

(Courtesy of Evelyn Acham)

(Courtesy of Evelyn Acham)

Kwa Evelyn, kuzungumza katika hafla na kuangaziwa na vyombo vya habari ni ishara kuwa amechukua mwelekeo mwema. “Linanitia moyo sana, kuona kuwa watu hawa wote wananihoji na kuwa ninahusika katika vikundi hivi vyote tofauti tofauti,” anasema. “Linanifanya nitambue kuwa sauti yangu inakuzwa zaidi.”

Lakini kufanya kazi kama mwanamke wa Kiafrika katika vuguvugu la kutetea hali ya hewa inaweza kuwa changamoto. “Sauti za Kiafrika hazijawakilishwa vya kutosha” Anasema Evelyn. Anakumbuka mwezi Januari mwaka huu, shirika la habari la Associated Press lilikata picha ya Vanessa kutoka kwa picha aliyokuwa miongoni mwa wenzake wa kizungu katika kongamano la wanahabari nchini Uswizi. Kwa Evelyn, jambo hilo lilikuwa mfano wa tukio la vuguvugu la watetezi wa hali ya hewa kudhalilisha juhudi za watu weusi na haswa wanaharakati wa Kiafrika. “Hawakufuta tu mtu mmoja bali walifuta bara zima,”anasema. Bali na kuwakilishwa, Evelyn anaamini katika kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa na matatizo ya ubaguzi wa rangi kwa pamoja — hasa sana katika Marekani ambako “ asilimia kubwa ya watu weusi wanaishi katika maeneo yaliyo machafu na yenye takataka hatari. … Wachafuaji hawaelekezi tu viwanda vyao katika maeneo yaliyo na kipato cha chini, bali pia wanachagua makusudi maeneo yaliyo na asilimia kubwa ya watu weusi.” Kutenganisha matatizo haya ni vigumu; “haki za Hali ya Hewa na Ubaguzi wa rangi kwa vyovyote vile,” anaeleza.

haki za Hali ya Hewa na Ubaguzi wa rangi kwa vyovyote vile
— Evelyn Acham

Akitazama mbele, Evelyn anatarajia kazi yake na Vanessa itaweka mfano wa hali ya mshikamano miongoni mwa wanaharakati wa hali ya hewa wa Uganda. “Vichwa vingi ni bora kuliko kimoja,” anashauri. Kwa vijana ambao tayari wamechukua hatua ya kutetea mazingira, ninataka kuwahimiza waendelee na kutia bidii wala wasikate tamaa. Watafute watu wenye sera kama yao, kama nilivyofanya na kubadilishana mawazo.”

Kwa sasa hayuko tayari kulegeza msimamo. Mwaka ujao Evelyn anapanga kuzindua +1 TreeUg, mpango wa kupanda miti milioni tisa nchini Uganda — mti mmoja kwa kila nyumba katika nchi. “Unaonekana kuwa mkubwa, lakini unawezekana,” anasema. “Kila jambo huanza kwa kufikiria, kisha kuamini, kisha kuliweka kwa vitendo.” Safari iliyo mbele ni ndefu, lakini Evelyn anaamini mpango wake utabadilisha Uganda kuwa bora: “Halitaisha kwa mwaka mmoja, utakuwa ni mradi unaoendelea. Ni bora kuanza kuliko kutoanza kamwe.”

Nakala hii ni kulingana na mahojiano na Evelyn yaliyofanywa na shirika la Malala Fund communications Mwenzi wa Omolara Uthman.

flower.png
Meet the Author
Meet the Author
Marielle Issa

(she/her) is a former editorial associate at Malala Fund. She loves cold weather, chocolate croissants and the novel “Little Women.”